BENKI YA NMB PANGANI YAADHIMISHA SIKU YA HUDUMA KWA WATEJA

Benk ya NMB tawi la PANGANI jana iliungana na wafanyakazi wengine wa Benk hiyo Duniani kote katika kusherehekea siku ya huduma kwa wateja kwa kushiriki chai ya pamoja ili kubadilishana mawazo na kuboreshewa huduma zao.

Meneja wa  Benki ya NMB Tawi la Pangani Bwana ABEL CHITOJO amesema kuwa lengo la kuadhimishwa kwa siku hiyo ni kuwaweka wateja wao karibu na kuwahudumia wote bila kujali matabaka.

Aidha Meneja huyo alisema kuwa kwa sasa wameweka utaratibu ambao Halmashauri zinaweza kukopa pesa au kupata misaada kwa ajili ya kununulia vifaa vya hospitali na vya shule ili kusaidia jamii yao katika masuala ya kimaendeleo hapa nchini.
Pia meneja huyo alisema kuwa kwa sasa NMB imeongeza huduma ya kubadili fedha kwa nchi za Afrika Mashariki ili kurahisisha ubadilishaji fedha kwa nchi hizo tatu ambazo ni Tanzania,Kenya,na Uganda, huku akitanabaisha kuwa huduma ya master card imeshaboreshwa.

Kwa upande wake Afisa Utumishi wilaya ya Pangani Bi MWANAIDI RAMADHANI NONDO akizungumza kwa niaba ya wafamyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani amesema kuwa Benki ya NMB inawasaidia sana wakazi wa Pangani na huduma zao ni nzuri na wanazipata kwa wakati.

Katika suala la mikopo inayotolewa na benki hiyo, Bi MWANAIDI alisema kuwa atalifikisha katika uongozi wa Halmashauri ili waweze kuitumia fursa hiyo ya kukopa kwa ajili ya huduma za kijamii kama vile vifaa vya Hospital na vya mashuleni.

Ambapo pia aliutaka uongozi wa Benki hiyo kusogeza huduma ya wakala wa kibenki katika shule ya sekondari hasa Tongani iliyopo kata ya Mkalamo ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi na walimu kuja Pangani Mjini kwa ajili ya kufuata huduma za kibenk.

Maadhimisho hayo ya siku ya huduma kwa wateja Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo mwezi wa kumi na Benk ya NMB kila, ambapo kauli mbiu ya siku hiyo inasema NMB TUNAJALI.

No comments

Powered by Blogger.