"WANANCHI WA PANGANI WANAPASWA KUTUNZA UOTO WA ASILI"- DAUDI MLAHAGWA



Wananchi wilayani Pangani wametakiwa kutunza uoto wa asili katika fukwe za bahari ili kupunguza kasi ya kusogea kwa bahari ambayo inatokana na kuliwa kwa ufukwe huo.

Agizo hilo limetolewa na Afisa Mazingira Wilaya ya Pangani Bwana Daudi Mlahagwa ambapo mbali na hilo lakini pia amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuuheshimu uoto huo ikiwemo Milakasa ili kuzuia bahari isiendelee kumeza ardhi kwa kuwa hali  ilivyo sasa inatishia kutoweka kwa mjini wa Pangani kutokana na kusogea kwa bahari hiyo.

Katika hatua nyingine Bwana Mlahagwa amesema kuwa kutokana na kasi hiyo ya bahari kusogesa karibu na mji wa Pangani jitihada walizozifanya ni kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira na rasilimali za bahari pamoja na  kuwaalika viongozi wakubwa wa serikali akiwemo Mheshimiwa Januari Mamkamba ambaye Mazingira na Muungano ili kusaidia ujenzi wa ukuta katika ufukwe huo.

Kasi ya kuliwa kwa fukwe za bahari imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na kuzua hofu ya kuzama kwa mji wa Pangani, lakini tayari serikali imeonyesha nia ya kudhibiti hali hiyo.


No comments

Powered by Blogger.