WANAKIKUNDI CHA UPENDO ENEO LA BOZA WALALAMIKIA HUDUMA YA MAJI KWENYE KILIMO CHA MBOGAMBOGA
Wajumbe wa kikundi cha
UPENDO kinachojihusisha na shughuli ya kilimo cha mbogamboga katika kijiji cha Boza wameelezea kuathiriwa
na kitendo cha mamlaka ya maji mjini Pangani kutofungua maji kwa wakati pamoja
na mifugo kuingizwa katika bustani zao hali inayosababishaa mbogamboga hizo kukauka.
Wakielezea kuhusu
changamoto zinazowakabili wakati walipotembelewa na mwenyekiti wa kijiji hicho
wajumbe hao wamesema kuwa upatikanaji wa maji umekuwa sio wa uhakika kwa sababu
utaratibu wa kupata maji ni siku tatu kwa wiki lakini kuna baadhi ya wasimamizi
hufungulia maji kwa muda mfupi na kupelekea athari za kupungua kwa kiwango cha
uzalishaji wa mazao huku wakilazimika kulipia bili ya maji kila mwez.
Aidha mbali na
changamoto ya utokaji wa maji kuwa siyo mzuri wanakikundi hao wamesema uingizwaji wa mifugo katika bustani
zao nayo imekuwa ni changamoto inayorudisha nyuma ukuaji wa mazao yao na kupelekea kupata mavuno machache ambapo
wamemuomba mwenyekiti wao awasaidie kutatua changamoto hizo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana SHABANI SUFIANI MUSSA amewapongeza wanakikundi
hao kwa kuanzisha mradi huo na kusema changamoto walizompa atazifanyia kazi kwa
kufika kwa meneja wa mamlaka ya maji
mjini Pangani ili ikiwezekana afike naye katika mashamba hayo kwa ajili
ya kutatua kero hiyo akisema wanakikundi hao wamekuwa wakilipa bili ya maji
wakati huduma hawaipati kwa usahihi.
No comments