UZIKWASA 'WAINOA' VMAC KIJIJI CHA MWEMBENI KUHUSU MALEZI NA MAKUZI YA MTOTO WA KIKE
Wajumbe wa kamati ya VMAC kijiji cha Mwembeni wamewataka
wazazi na walezi wilayani PANGANI kuachana na tabia ya kuwatoa
wanafunzi mimba na badala
yake kuwasimamia katika makuzi na
malezi bora ili waweze kuwa na ustawi
mzuri wa elim.
Akizungumza
mara baada ya mafunzo ya
kuibua changamoto za ukatili wa
kijinsia kwa wanawake, wasichana na watoto
yanayotolewa na shirika la UZIKWASA mwenyekiti wa kamati hiyo Bi PILI
YUSUPH ameahidi kushirikiana na wanakamati
kuwabaini wanaoshiriki katika vitendo
hivyo na kuwachukulia hatua za kisheria
na kuwataka kuaacha mara moja kwani inahatarisha afya za watoto.
Nae Bwana JUMAA SABURI ambaye ni mjumbe wa kamati
hiyo amesema kuwa vitendo hivyo ni vichafu mbele ya Mungu na pia
wanafunzi ni lazima wawe makini
kwani jamii inawategemea katika kuwapata wataalamu wa fani mbali mbali
hapa nchini .
Katika hatua nyingine wajumbe wa
kamati hiyo wameahidi kuweka mikakati madhubuti ya kupambana na matukio
yote ya ukatili ikiwemo suala la vipigo
kwa wenza ubakaji katika ndoa na utumikishwaji kwa watototo wadog.
Hayo yote yamejiri katika mafunzo ya kupinga ukatili
ambayo yanawawezesha kwa pamoja viongozi kuzama kujitafiti na kuibua matukio ya
ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na
watoto na kuweka mpango wa pamoja jinsi ya kumaliza matukio hayo
No comments