WANANCHI KIJIJI CHA MWEMBENI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA VMAC
Wananchi wa kijiji cha MWEMBENI wametakiwa kushirikiana
na wajumbe wa kamati ya VMAC
kijijini hapo ili kutokomeza
matukio ya ukatili yanayowakabili wanawake wasichana na watoto
kijijini hap.
Akizungumza
na Pangani Fm Mwenyekiti wa kijiji
hicho bwana MWELEKA MAHIMBURA
mbali na kuwataka
wananchi kushirikiana na
wajumbe katika kupunguza
matukio hayo amewaomba
wajumbe wakamati kuondoa dhana
ya kuwa jukumu la kutekeleza
mpango kazi waliojiwekea ni la
mtendaji na mwenyekiti pekee.
Kwa upande wake
muwezeshaji kutoka shirika
la UZIKWASA ambaye pia ni mratibu wa masuala ya jinsia
Bi SALVATA KALANGA amewataka
wajumbe hao kufanya juhudi za kukemea matukio ya ukatili popote walipo
ikiwemo kwenye nyumba za ibada ,vijiweni
na hata kwenye
mikutano ya vijiji.
Hayo
yamejiri katika mfululizo
wa mafunzo ya kupinga
ukatili wa kijinsia yanyoendelea
kijijini hapo ambapo
changamoto zilizoibuliwa kwa siku
yakwanza zinatarajiwa kufikishwa
kwa wananchi kwa njia ya
sanaa za maigizo siku
ya mwisho ya mafunzo hayo.
No comments