MWANAMKE AENDA JELA MIEZI 13 PANGANI KWA WIZI WA SIMU



Mahakama ya mwanzo wilayani Pangani imemuhuku Bi FATUMA RASHIDI mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa KIPUMBWI kwenda jela miezi 13 kwa kosa la wizi wa simu aina ya Tecno W3.

Hati ya mashtaka inaeleza kuwa Bi Fatuma ametekeleza tukio la wizi wa simu aina ya Tecno W3 rangi wa silver yenye thamani ya shilingi laki moja na elfu tisini, tarehe 13/9/2017 majira ya saa sita kamili mchana alipokuwa hotelini.

Imeelezwa kuwa  Bi Fatuma alifika hotelini maarufu KWA MAMA MAKWARUZO iliyopo mtaa wa USALAMA kata ya PANGANI MASHARIKI ambapo alifika kama mteja wa kawaida hotelini hapo, baada ya muda Bi Fatuma aliiona na kwenda kuichukua simu hiyo mali ya Bi MAGRETI LUCAS ambapo alikuwa ameisahau baada ya kumaliza kupata chakula.

Baada ya kusomewa na kukubali shtaka hilo la wizi wa simu, Hakimu wa mahakama hiyo bwana JORDAN MULINDA alimuhukumu B i FATUMA RASHIDI kwenda jela miezi kumi na tatu au kulipa faini ya shilingi laki tatu(300,000).

Bi Fatumu Rashidi amehukumiwa kwenda jela miezi kumi na tatu baada ya kushindwa kulipa faini aliyotakiwa kuilipa mahakamani baada ya kutekeleza tukio la wizi mapema hapo jana.

1 comment:

Powered by Blogger.