CCM WILAYANI PANGANI WAFANYA UCHAGUZI
Jumuiya ya wazazi wilayani Pangani mkoani Tanga
mwanzoni mwa wikii hii imefanya uchaguzi wa viongozi wa jumuiya hiyo ili kupata
viongozi wa ngazi mbali mbali.
Akizungumza na Pangani Fm radio ofisini kwake katibu
wa chama cha mapinduzi CCM wilayani humo Bwana Salum Mtelela amesema mchakato
wa uchaguzi huo umekwenda vizuri huku akipongeza wanachama wa chama hicho kwa
kujitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi za uongozi jambo ambalo limepelekea
uchaguzi kuwa mwepesi, huru na haki katika kufanya maamuzi ya kumchagua
kiongozi unayemtaka.
Kwa upande wa washindi katika uchaguzi huo ambaye ni
Bi.
Pili Mrefu Makwaruzo kwa nafasi ya Mwenyekiti
wa jumuiya ya wazazi na Bi. Imma Omari Kipalo kwa nafasi ya katibu elimu
na malezi, wameonekana kufurahia ushindi huo huku wakiahidi kufanya kazi kwa
bidii.
Wajumbe waliopata nafasi katika mkutano mkuu kitaifa
ni Bi. Amina Abdallah Mwaupea, huku mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha
mapinduzi (CCM) Wilaya ya Pangani ni Bi. Mwanaidi Suleimani Mussa na Bwana Kasimu
Saidi Omari kwa nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wazazi mkoa wa tanga.
Bwana Mtelela ameendelea kutaja mjumbe wa kuwakilisha
kutoka wazazi wa (UVCCM) ambaye ni Bwana. Hassani Muina Kadogo huku mjumbe mmoja
kutoka wazazi kwenda UWT ni Bi. Pili Alli Msabaha.
Mwisho amemalizia kwa nafasi ya wajumbe watatu wa
baraza la wazazi wilaya ya Pangani kuwa ni Sungura H. Kamaga, Mwantumu S. Makuka
Na Mwanahamisi Saidi Rashidi.
No comments