MBUNGE WA PANGANI AWAASA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA WANAOANZA MITIHANI YAO LEO
Mbunge wa jimbo la Pangani Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso
amewaasa wanafunzi wote wanaotarajia kufanya mitihani ya darasa la saba jimboni
kwake kufuata sheria za mitihani hiyo ili kuhakikisha wanafanya vizuri mitihani
yao.
Akizungumza na Pangani Fm Mheshimiwa Awesso amesema
kuwa kufanya kwao vizuri kutawawezesha wanafunzi hao kuja kuwa wataalamu
mbalimbali kama vile madaktari, waalimu na hata fani nyingine mbalimbali.
Aidha Mheshimiwa Awesso amewataka wazazi kuwatia moyo watoto wao na pia kushirikiana vyema na waalimu
ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika salama.
Mbunge huyo pia amesema atashirikiana na serikali
ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu wilayani Pangani
ikiwemo uhaba wa waalimu na hata miundombinu rafiki ya kufundishi.
Mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi unaanza leo kwa
shule zote za msingi ambapo mitihani hii itawawezesha wanafunzi watakao
chaguliwa kujiunga na shule za upili.
No comments