ULEVI WA KUPINDUKIA UMEELEZWA KUWA NI CHANZO CHA UDHALILISHAJI NA UKATILI KWA WANAWAKE
Ulevi Wa kupindukia umeelezwa kwa chanzo kinachosababisha
udhalilishaji na ukatili kwa wanawake hasa katika maeneo ya vijijini.
Licha ya udhalilishaji kujitokeza pale ambapo
mwanamke mwenyewe anakwenda kilabuni na kulewa hadi kufikia hatua ya kutojitambua
na kujikuta akifanyiwa vitendo vya kikatili kama kuliwa mande, vitendo vitendo
ambavyo vimekuwa vikijitokeza sana katika maeneo ya vijijini.
Bi Adelina Rajabu ambae ni mkazi wa kijiji cha
Kigurusimba Wilayani Pangani ni miongoni mwa wale waliowahi kupigwa na mumewe
huku chanzo akieleza kuwa ni ulevi.
Bi Adelina ameieleza Pangani fm kwamba mara nyingi
mumewe anapokuwa amelewa amekuwa akimtoloea maneno ya kumsimnga na kumtaka
arudi nyumbani kwao, licha ya kuwa baada ya mumewe kumtolea maneno hayo amekuwa
akifungasha mabegi na kujibanza pembeni na nyumba yake kwa lengo la kusubiri
mumewe apunguze hasira kisha kurudi nyumbani kwake na kuendelea kuwepo nyumbani
hapo.
Pamoja na mume wa Adelina kuwa na tabia ya masimango
kila amapolewa sasa imefikia hatua ya kumchapa mkewe kwa fimbo kama mtoto hali
iliyopelekea Bi adelina kupata maumivu makali mwilini wake, lakini kwa sasa Bi
Adelina ameamua kurudi nyumbani kwa wazazi wake ili apumzike.
Mama mzazi wa Adelina BI MWAJUMA DAUDI ameeleza
kusikitishwa na tukio hilo na kuchukua hatua ya kutoa taarifa kwenye uongozi wa
kijiji.
Bi Mwajuma amewataka wanaume wote wenye tabia ya
kuwapiga au kuwafanyia vitendo vya kikatili wanawake kuacha tabia hiyo kwani
kufanya hivyo ni kushusha thamani na hadhi ya mwanamke.
Licha ya BI ADELINA kumsamehe mumewe kwa kitendo cha
kumchapa kwa sasa ameamua kuishi nyumbani kwa wazazi wake hadi pale maumivu
yatakapoisha
No comments