MWANAMKE AENDA JELA KWA KUPATIKANA NA HATIA YA KUOLEWA MARA MBILI
Mahakama ya
mwanzo ya Mwera imemuhukumu Asha Hassani mwenye umri wa miaka 32 mkazi
wa Langoni, kwenda jela miezi 9 ama kulipa
faini ya shilingi laki 5 baada ya
kupatikana na hatia ya kuolewa mara mbili.
Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo ya
Mwera Anthon Hamza amesema mtuhumiwa
huyo alitenda kosa hilo la kuolewa na mwanaume mwingine huku akifahamu kwamba
yeye ni mke wa mtu kutokana na ndoa yake na mumewe wa kwanza ikiwa bado
haijavunjika.
Katika hati ya mashataka iliyowasilishwa na polisi
mahakamani hapo ilidaiwa kuwa mnamo tarehe 29 mwezi wa 5 majira ya saa mbili na
nusu usiku huko Langoni Bi Asha aliolewa
na Bwana DUNGU OMARI, ambapo mwanzo kabla ya hapo alikuwa ameolewa na Bwana
DOTTO JUMA, na hii ilikuwa ni tarehe 5 mwezi wa 5 mwaka 2002 ndoa
iliyofungishwa na Sheikh Mohamed Ally Muhaka.
Kutokana na ndoa ya awali kuwa bado
haijavunjika kwa hati ya talaka kwa
mujibu wa sheria za kiislamu basi imeonekana ni kosa kwa Bi ASHA HASSANI
kuolewa hali ya kuwa alikuwa bado ni mke wa mtu kisheria, na baada ya hukumu
hiyo mtuhumiwa huyo alishindwa kulipa faini hiyo hivyo kwenda jela miezi hiyo
tisa.
Mahakama hiyo pia imemuhukumu Bwana Twaha Rajabu
mkazi wa mkalamo mwenye umri wa miaka 23 kwenda jela miezi mitano au kulipa
faini ya shilingi laki tatu na nusu, baada ya kupatikana na hatia ya kumtishia
mtu kwa silaha aina ya sime.
Katika hati ya mashataka iliyowasilishwa na polisi
mahakamani hapo ilidaiwa kuwa mnamo tarehe 8 mwezi wa 8 majira ya saa moja
huko Mkalamo Bwana Twaha alimtishia
Bwana Jumanne Juma kwa sime,na baada uendeshwaji wa kesi hiyo mahakama ilimkuta
na hatia kijana Twaha Rajabu,ambapo alishindwa kulipa faini hiyo ya shilingi
laki tatu na nusu na kwenda kutumikia kifungo hicho cha miezi mitano gerezani.
No comments