VMAC YA MASAIKA YAIPIGA 'TAFU' KAMBI YA DARASA LA SABA KIJIJINI HAPO
Kamati ya kudhibiti ukimwi VMAC ya kijiji cha
Masaika leo imeichangia kambi ya masomo ya darasa la saba ya shule ya msingi masaika kiasi cha shilingi
29,500 kwa ajili maandilizi ya mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi kiasi hiko cha
fedha,mjumbe wa kamati hiyo Bwana BAKARY MWAROGO amesema kuwa lengo la
kuwasaidia ni kutaka kuwapa motisha ili wafanye vizuri katika mitihani yao ya
kuhitimu elimu ya msingi.
Naye kwa upande wake mwalimu athumani Mgeni ambaye
ni mwalimu wa shule hiyo Ameongeza kuwa anaishikuru kamati hiyo kwa kusaidia
fedha hizo,Hali itakayopelekea kupata aina mbali mbali ya chakula jambo ambalo
litafanya wanafunzi hao kufanya vyema katika mitihani yao ya taifa.
Shule mbali mbali wilayani pangani zimekuwa
zikiwaweka kambi wanafunzi wa darasa la saba kwa ajili ya kufanya vyema katika
mitihani yao ya mwisho.
No comments