VMAC YA KIJIJI CHA MIVUMONI YATOA MCHELE KWA SHULE YA MSINGI
Kamati ya kudhibiti Ukimwi ya kijiji cha Mivumoni
hii leo imetoa Msaada wa mchele Kilo 23
kwa wanafunzi wa Darasa la saba shule ya msingi Mivumoni kama chachu ya kufanya vizuri katika mitihani
yao ya mwisho.
Akizungumza na Pangani fm wakati akikabidhi chakula
hiko , mwenyekiti wa kijiji hiko Bwana Venasi Onesmo amesema kuwa lengo la
kutoa chakula hiko ni kuwapa motisha wanafunzi hao kujifunza zaidi hali
itakayopelekea kujiaanda vyema na mitihani.
Mbali na kugawa mchele huo, kamati hiyo pia imeanza
ujenzi wa choo katika ufisi ya kijiji cha Mivumoni kwa ajili ya kuweka
mazingira mazuri.
Kwa upande wao wanafunzi wa darasa la saba wa shule
hiyo wameshukuru kwa kupewa mchele na kuahidi kufanya vizuri katika mitihani ya
mwisho.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Ndugu Kalage Zahoro
licha kutanabaisha kuwa tangu waanze kambi
ya masomo ratiba yao ilikuwa ugali na mapure,Pia ametoa shukrani kwa
msaada huwo wa chakula huku akisema matumaini yake wanafunzi hao kufanya vyema.
Kamati za kudhibiti ukimwi zinazoratibiwa na shirika
lisilo la kiserikali uzikwasa zimekuwa zikichangia misaa mbali mbali katika shule za msingi na
sekondari wilayani pangani kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu wilayani
pangani.
No comments