WANANCHI PANGANI WATAKIWA KUTII SHERIA BILA YA SHURUTI
Wananchi wilayani
Pangani wametakiwa kuendelea kutii sheria bila shuruti katika sehemu zao
wanazoishi ili kuhakikisha usalama na
amani unaendelea kuwepo kwa sababu suala hilo ni endelevu na halina kikomo.
Wito huo umetolea leo
na Mkuu wa polisi wilaya ya Pangani Bi Christina Musyani kutokana na kuonekana
baadhi matendo ya uhalifu na uvunjaji wa sheria zilizowekwa ikiwemo matukio kwa
baadhi ya wanaume kuwapa mimba watoto wadogo pamoja na baadhi ya Bodaboda
kutofuata kanuni za uendeshaji vyombo hivyo.
Akizungumza na Pangani
fm Mkuu huyo wa Pilisi amesema kuwa vitendo vya baadhi ya wanaume kuwapa mimba
wasichana wadogo, kulawiti, ubakaji na kupiga ni vitendo visivyompendeza Mungu
na hata katika jami, hivyo inawapasa kujirekebisha huku akisema jeshi la polisi linachukizwa na vitendo hivyo
na litawafuatilia watu wote wanaotekelza matukio hayo ili hatua kali
zichukuliwe dhidi yao.
Pia aliwataka wanajamii
kuwalinda wanafunzi wakati huu wa likizo ili kuhakikisha shule zinapofunguliwa
warudi wakiwa salama na kuendelea na masomo yao.
Aidha Bi Musyani
amewataka waendeshaji wa vyombo vya moto kuzingatia kanuni za usalama wa
barabarani kwani waljifunza katika mafunzo yao ya udereva na kuwaonya baadhi ya
waendesha pikipiki nyakati za usiku bila
kuwasha taa pamoja na kuzingatia muda wa mwisho wa kufanya kazi ya
kusafirisha abiria ambao ni saa 4 usiku akionya kuwa hatua kali zitachukuliwa
kwa yeyote atakayekiuka.
Kumekuwa kukitokea
matokea matukio ya uvunjifu wa kanuni za usalama barabarani, ubakaji pamoja ulawiti
kwa watoto katika baadhi ya maeneo
wilayani Pangani kunakotajwa kusababishwa na malezi yasiyofaa kwa baadhi ya
wazazi.
No comments