KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA HABARI TANZANIA BWANA KAJUBI MUKAJANGA ATEMBELEA PANGANI FM



Katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania bwana KAJUBI MUKAJANGA jana alitembembea shirika lisilo la kiserikali la UZIKWASA lililopo wilayani PANGANI pamoja na kituo cha radio cha PANGANI FM kinachomilikiwa na shirika hilo kwa lengo la kukabidhi nakala mbali mbali zilizozalishwa na baraza hilo.


 Bwana Kajubi amemkabidhi meneja wa kituo Bi MAIMUNA MSANGI, nakala mbili za katiba la barazala la habari, nakala mbili za azimio la dar es salamu juu ya uhuru wa uhariri na uwajibikaji, ripoti ya mwaka 2016 juu ya ufuatiliaji wa hali ya vyombo vya habari na matukio yanayokumba vyombo hivyo Tanzania na Zanzibar iliyosheheni masuala ya elimu na sheria (state of the media).



Ameongeza kuwa baraza la habari Tanzania linasimamia kanuni na maadili kwa vyombo vya habari hivyo alimkabidhi meneja wa kituo hicho nakala ya kanuni iliyochapishwa  agost 31 mwaka huu pia amemalizia kwa kusema kuwa moja ya majukumu yao ni kuchunguza, kupeleleza  na kutoa taarifa za matukio yaliyoingilia haki ya habari na haki ya uhariri, hivyo alikabidhi ripoti iliyohusiana na uzuiaji wa kurusha moja kwa moja taarifa za bunge ijulikanayo kama ‘’nchi yetu bunge letu’’

Nao  wanahabari wa pangani fm radio walipata nafasi ya kuzungumza na bwana KAJUBI mambo mbali mbali ikiwemo masuala ya ushiriki wa tunzo za waandishi habari mahiri kupitia MCT huku akiwatoa wasiwasi kuwa baraza la habari linaamini waandishi kutoka mikoani ni waandishi bora hivyo wafanye kazi kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.

1 comment:

Powered by Blogger.