MATUKIO YA UKATILI YAPUNGUA MKWAJA, HUKU MATUMIZI YA KONDOMU KWA VIJANA YAKIIMARIKA
Wananchi wa kijiji cha MKWAJA wilayani Pangani wameeleza
kupungua kwa matukio ya ubakaji na ulawiti katika kijiji chao ambayo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara.
Wakizungumza na Pangani Fm wananchi, pamoja na mambo
mengine pia wameipongeza kamati yakudhibiti ukimwi ya kijiji hicho kwa
kuyashughulikia matukio ya ulawiti na ubakaji yaliyokuwa yakijitokeza hali
iliyosaidia kupungua kwa vitendo hivyo viovu.
Katika hatua nyengine vijana wa kijiji hicho pia
wameipongeza kamati hiyo kwa kuelimisha jamii juu ya matumizi ya kondomu huku wakisema kwa sasa kasi ya utumiaji imeongezeka.
Vijana hao wameeleza kuwa hapo awali haikuwa rahisi
kwao kukubali matumizi ya kondom lakini kutokana na juhudi za kamati hiyo
kuielimisha jamii hasa vijana , mabadiliko yameanza kuonekana.
No comments