USIRI WA UTOAJI WA TAARIFA ZA UHALIFU BADO CHANGAMOTO KIJIJI CHA KIMANG'A
Baadhi ya vijana kijiji cha Kimang’a wilayani Pangani,
wameelezea kinachosababisha wao kushindwa
kutoa taarifa kwa wazazi wa watoto wanaotumia dawa za kulevya kutokana na
kueleweka vibaya kwa jamii.
Vijana hao wasema kuwa baadhi ya wazazi kijijini
hapo wamekuwa na upendo wa kupitiliza kwa watoto wao kiasi cha kushindwa
kuamini kile kinachoelezwa kuhusu watoto wao kutumia dawa hizo.
Wameongeza kwa kusema kuwa hata kwa upande wa jeshi
la polisi baadhi yao wanakosa kuwa na usiri pindi wanapowapa taarifa hizo, na
badala yake mtoa taarifa hujulikana.
No comments