WATOA HUDUMA ZA KIJAMII PANGANI WATAKIWA KUZINGATIA TARATIBU ZA KIAFYA ZILIZOWEKWA
Afisa wa afya wilaya Pangani Bwana JOHSEPHAT MAKOMBE
amewataka watoa huduma za jamii kufuata masharti ya kisheria kama walivyoagizwa
ili kuepukana na usumbufu wa kufungiwa biashara zao.
Akizungumza na Pangani Fm Bwana MAKOMBE amesema kwa
sasa wapo katika zoezi la kufungia biashara ambazo hazikutimiza masharti
waliotoa huku akifafanua vigezo vinavyo takiwa ili kukidhi kundesha huduma za
jamii ikiwemo saluni.
Bwana MAKOMBE amesema vigezo hivyo ni chumba,
ambazho kiwe na mwanga wa kutosha, kifaa cha kuzimia moto, sanduku la huduma ya
kwanza, na kuwa na dawa za kusafishia vifaa hivyo.
Aidha MAKOMBE ameweka wazi suaala la kupima afya
kuna fomu maalum zinazojieleza upimaji wa magonjwa, huku akisema kupima Ukimwi
ni suala la maamuzi ya mhusika mwenyewe.
No comments