BODA BODA FC YAENDELEZA UBABE KWA CHELSEA YA BOZA
Ligi ya AWESSO
CUP inayoendelea kurundima katika kijiji cha Boza wilayani Pangani, imetimua
vumbi katika viunga vya Uwanja wa mpira
shule ya msingi Boza, katika mchezo uliowakutanisha Boda Boda Fc na
Chelsea ya Boza.
Mpaka dakika tisini ya mchezo Boda Boda imewacharaza
bao 2 kwa 1 timu y Chelsea fc, mabao ya timu ya Boda boda yamewekwa kimiani na Ngongo
Mbwana mnamo dakika ya 61 Na Seiph Mwakijo Dakika ya 84 huku bao la kufutia
machozi la timu ya Chelsea likifungwa na Juma Bakary.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo unaowakutanisha
RENGERS STAR ya mwembeni na CHOBA STAR ya choba.
No comments