MAFUNZO YA UONGOZI WA MGUSO YAZAA MATUNDA KATIKA KIJIJI CHA MIKINGUNI
Mafunzo ya uwongozi wa mguso yameonekana kuwa na
tija yenye kuleta maendeleo chanya katika uwongozi wa kijiji cha Mikinguni
Wakizungumza na pangani fm wajumbe wa kamati ya
kudhibiti ukimwi ya Mikinguni wamesema kuwa,awali kabla hawajapatiwa mafunzo ya
uwongozi wa mguso,walikosa nguvu mbadala ya kushirikiana na jamii
inayowazunguka na kupelekea kuibuka kwa migogoro mbali mbali katika kijiji
chao,lakini tangu wapewe elimu ya uwongozi wa mguso na shirika la Uzikwasa
wameweza kutatua migogoro mbali mbali iliyopo kijijini hapo na kupelekea
kujenga umoja kati ya viongozi na jamii husika.
Mbali na hayo muwakilishi kutoka katika jamii ya
kifugaji ya kimasai bwana Moleli ambaye yeye pia ni mjumbe wa kamati
hiyo,amesema kuwa kabla ya kupatiwa mafunzo hayo alikuwa anatumia mfumo dume
katika jamii yake ya kimasai kama baba na kutumia mabavu katika maamuzi,lakina
tangua ajue uwongozi wenye mguso,umemuwezesha kutoa fursa kwa wake na watoto
zake kuzungumza hali inayoepusha migogoro katika familia yake
Naye kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hiko bwana
salum Bungala ambaye pia mjumbe wa kamati hiyo,ametanabaisha anajiona amezaliwa
upya baada ya mafunzo,na kuongeza kuwa mafunzo hayo yamemuwezesha yeye kama
kiongozi kutambua uwezo na nguvu uliyondani yake jambo linalopekea kuchuku
maamuzi stahaki pale kunapotokea changamoto kijiji hapo.
Mafunzo haya uwongozi wa mguso ni mafunzo
yanayoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la Uzikwasa,ni mafunzo yenye
lengo la kumuwezesha kiongozi mmoja mmoja,kujitambua na kutatua changamoto
zinazomzunguka kwa kutenda haki na usawa.
No comments