HATIMAE JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI LAZINDULIWA PANGANI
Wanawake Wilayani Pangani wamefanya hafla ya
kuzindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa kupiga kura iliyowezesha
kuwapata viongozi watakao wawakilisha katika jukwaa hilo.
Jukwaa hilo linalenga kuwakutanisha wanawake ,kujadili
fursa,changamoto na na jinsi ya
kushiriki kikamilifu katika biashara na
shughuli nyengine za uchumi ,vilevile kuongeza uwelewa wa wanawake hao katika
masuala ya kiuchumi.
Waliochaguliwa kuwa viongozi wa jukwaa hilo ni Bi
Manusa Bakari kwa nafasi ya mwenyekiti, na BI Fatuma Issa kwa nafasi ya makamu
mwenyekiti.
Katibu ni Bi Akida Sabiri Masanga,na katibu msaidizi
ni Bi Mwantumu Makuka.
Mweka hazina ni Bi Hawa Kizamba
Wajumbe
wa kamati tendaji ni ;-
1. Matingisa
Hamza
2. Mwanasha
Rajabu
3. Priscar
Zakari
4. Mwantumu
Rajabu
5. Mwanaidi
Omari
No comments