VMAC YA KIJIJI CHA MWEMBENI YAHITIMISHA MAFUNZO KWA KISHINDO
Wananchi wa kjijiji cha Mwembeni wametakiwa kuachana na mila ambazo zinamkandamiza na kumdhalisha mwanamke
na mtoto wa kike kijijini
hapo na badala yake kujali utu na thamani ya mwanamke.
Akizungumza
mara baada ya tamasha la jinsia
lililofanyika kijijini hapo mjumbe wa
kamati ya VMAC Bwana JUMAA SABURI mbali
na kutaka jamii kuachana na mila kandamizi
ameshauri kuendeleza mila ambazo
zinazingatia utu na thamani ya mwanamke katika jamii.
Akichangia
mjadala ambao uliibuka mara
baada ya tamasha hilo Bi SIKUDHANI LASMOS ambaye ametokea katika kabila la kimakonde
amesema kuwa yeye hayupo
tayari kuacha mila zake ambazo ni lazima
binti kutolewa nje huku akiwa
matiti yako nje na kudai kuwa utamduni huo ulikua tangu zamani na haukuleta athari zozote kikubwa ni mabinti kujitunza na kuthamini utu wao.
Nae bi fatma chonya amewasihi wanajamii hiyo
kuachana na mila kandanizi
kwaani binti kumtoa nje huku sehemu ya matiti
inakuwa wazi ni udhalilishaji wa
kijinsia na kuongeza kuwa kitendo hiko kinaonngeza matamanio
kwa wanaume hali ambyo inaweza kuhgamasisha vitendo vya ubakaji.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana
MWELEKA MAHIMUBURA amewataka wanachi kushirikiana na viongozi
katika kuondoa matuko ya ukatili
kijijini hapo.
Hayo yamejiri katika tamati ya mafunzo ya jinsia yanayotolewa
na shirika la uzikwasa kwa siku nne mfululizo lengo likiwa ni kuibua
changamoto za ukatili kwa
wanawake na watoto na kuweka mikakati ya pamoja kati ya viongozi na wananchi.
No comments