WANAKIKUNDI WA KIKOBA CHA MWINDAU FOUNDATION WAHAMASIKA KUCHANGIA DAMU
Wanakikundi wa kikoba cha mwindau foundation kilichopo katika kata ya Bushiri kijiji cha msaraza Wilayani pangani hii leo wamechangia Damu salama kwa ajili ya Kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu kama vile mama wajawazito na watoto.
Wakizungumza mara baada ya kuchangia damu salama
wamesema kuwa wamechangia kwa ajili ya kuokoa maisha ya wakina mama
wajawazito,watoto na wagonjwa wengine na kuitaka jamii iwe na moyo wa kuchangia
damu salama,Kwani hakuna madhara yoyote yanayoweza kuwakuta.
Kwa upande wao Kikundi cha kudhibiti ukimwi vmack
msaraza kupitia mwenyekiti wake Hemedi Daudi ambao walisaidia kuwapa elimu ya
uchangiaji damu kikundi cha bushiri wametanabaisha kuwa wamewahamasisha
kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu salama.
Bibie Muhamedi Suleiman ni mwenyekiti wa kikundi cha
mwindau foundation Ameongeza Kwa kuitaka jamii ya pangani Hususa ni wakinamama
kuwa na moyo wa kuchangia damu Kwani wao ndio wenye uhitaji mkubwa wakati wa
kujifungua.
Kwa kumalizia mjumbe wa kamati ya damu salama,ambaye
ni msimamizi wa zoezi hilo kutoka hospital ya wilaya ya pangani Bwana peter
mshabaha amesema zoezi la utoaji damu limeenda vizuri na kuwataka wananchi wawe
na muamko wa kuchangia damu.
Damu salama imekuwa ni muhimu sana hususa ni kwa
wakimama wajawazito hali inayopelekea,serikali kuwahamasisha wananchi kuchangia
damu ili kupunguza vifo vya wakina mama.
Timu ya damu salama ikiongozwa na mratibu wa damu
salama kutoka hospitali ya wilaya ya
Pangani Alhamisi wiki hii imefanikiwa
kuvuna chupa 16 za damu kwenye zoezi la
ukusanyaji wa damu kijiji cha Meka
kilichopo katika wilaya hiyo kwa lengo la kusaidia utoaji wa huduma kwa wenye
mahitaji ya damu ili kupunguza vifo
vitokananvyo na upungufu wa damu.
Akizungumza baada ya kuhitimishwa kwa zoezi hilo
katika kijiji cha Meka Mratibu wa damu salama wilaya ya Pangani Dokta Mfaume
Salehe amewashukuru uongozi wa kijiji
hicho pamoja na wakazi wote waliojitolea damu
kwa moyo wao wa uzalendo na kusema kwamba zoezi hilo litakuwa ni
endelevu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa
wenye mahitaji ya damu ikiwemo kinamama wajawazito.
Kwa upande wao wakazi waliojitokeza kuchangia damu
wameelezea kufarijika kwa kuwa wamechangia damu kwa ajili ya kuwasaidia
watanzania wenzao huku wakiwaomba wataalamu wa afya kutoa damu bila malipo
pamoja na kendelea kuwahamasisha wanajamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu
ili kupata akiba kubwa ya damu katika
hospitali hiyo.
Katika hatua nyingine Dokta Mfaume amesema ili
kuongeza kiwango cha ukusanyaji damu katika wilaya ya Pangani watafanya kampeni
ya kuhamasisha uchangiaji damu salama kuanzia tarehe 25 hadi 29 Mwezi huu wa
tisa mwaka 2017 huku akiwaomba wananchi wahamasike katika uchangiaji wa damu.
Katika wilaya ya Pangani kumeonekana wakazi wake
wameanza kuhamasika katika kuchangia
damu na kusaidia kupunguza changamoto ya wagonjwa kuhamishiwa hospitali ya
Bombo kwa ajili ya kupatiwa damu .
No comments