WANAFUNZI WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI KIMANG'A WAAHIDI KUFANYA VIZURI MTIHANI WAO WA MWISHO
Wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Kimang’a wilayani Pangani wameweka wazi maandalizi waliyofanya katika kuelekea kwenye mtihani wao wa mwisho wa Taifa unaowakabili utakaoanza kufanyika Agost 6 2017.
Wakizungumza na Pangani Fm wanafunzi hao mara baada ya kukamilisha baadhi ya maandalizi ya mtihani huo ikiwemo kusafisha madarasa pamoja na kupanga viti wamesema wamejiandaa vizuri na wanaamini wote watafaulu wote huku wakiweka imano yao kwa Mungu.
Wanafuni hao pia wanawashukuru wazazi na walezi wao kwa kuwapa muda wa kujisomea, pamoja na kuwaruhusu kwenda shule kujisomea masomo ya ziada wakati wa usiku huku wakiwapa ulizi ili kuepukana na matatizo ambayo wangeweza kukutana nayo,.
Nae mwalimu mkuu wa shule hiyo PETER DOMINICK CHAUSA amesema amewaandaa vya kutosha wanafunzi wake na anaamini wote watafaulu kwa kupata alama za juu, pia amewapongeza wazazi kwa kushirikiana vizuri katika kuwaandaa watoto hao.
Shule ya Shule ya msingi Kimang’a imejibebea umaarufu wilayani Pangani baada ya kijana SAID MATHIAS kushika nafasi ya kwanza kwenye somo la HISABATI kwa kupata alama 46 kwenye mtihani wa kujandaa na mtihani wa taifa (MOCK) kati ya wanafunzi wote wilayani humo.
ATTENTION : NECTA PSLE Primary school leaving examination Result 2019/20 are out !!!!
ReplyDeleteUse the following links to access Matokeo ya necta darasa la saba 2019
https://aucfinder.com/matokeo-ya-darasa-la-saba/