MUINGILIANO WA MAKABILA TANZANIA, FURSA NA CHANGAMOTO ZAKE
Muingiliano na mchanganyiko wa watu wa makabila
tofauti imeonekana kuchangia
kupotea kwa baadhi ya mila na
tamaduni za makabila mbalimbali hususani yale yaliyohamia kutoka mkoa mmoja
hadi mwingine.
Akizungumza na Pangani Fm Mzee Adam Manda ambae ni Mmakonde
kutoka mkoani Mtwara, amesema kwa upande wake muda ambao amekuja mkoani Tanga
ni katika kipindi ambcho alikuwa na umri wa miaka 10 kiasi cha kukosa fursa
nzuri ya kujifunza juu ya mila na tamaduni za kabila lake kwa undani kutokana
na kuishi na jamii nyingine.
Katika maelezo yake Mzee Adam Manda baada ya kuja
mkoani Tanga na kuishi katika wilaya ya Pangani huku akifanya kazi katika
shamba la mkonge, baadae aliiona kazi hiyo ni ngumu na ndipo alipoondoka na
kwenda nchini Kenya ambapo huko alijishughulisha na sanaa ya vinyago ambavyo
aliviuza katika hoteli za wazungu.
Wilaya ya Pangani ambayo makabila yake ya asili ni
wazigua na wabondei kwa sasa ina muingiliano wa makabila mbalimbali kama vile Wabena,Waha
,Wamakonde, Wabena na makabila mengine ambapo pamoja na muingiliano huo lakini
kila kabila linaheshimu kabila la mwenzake.
Hatu wapati vizuri online
ReplyDelete