KIJANA AENDA JELA KWA KUMTISHIA MTU MAISHA WILAYANI PANGANI
Mahakama ya mwanzo kata ya Mwera wilayani Pangani
imemhukumu kijana MOHAMED YASSIN (21) kwenda jela miezi kumi na mbili (12) kwa
kosa la kumtishia kwa silaha Bwana ABDALAH SHABAN.
Hati ya mashtakaowasilishwa mahakamani hapo ili
inaeleza kuwa mnamo tarehe 16/8/2017 majira ya saa nane kamili mchana mshtakiwa
alitaka amchome kisu Bwana Abdalah Shabani ambacho alikuwa amekiweka kwenye mfuko wa nguo alizokuwa amezivaa.
Baada ya mshtakiwa kusomewa shtaka hilo alikataa
kuhusika katika tukio hilo na ndipo mahakama ikasikiliza ushahidi wa pande zote
mbili na kumkuta mshtakiwa na kosa
lililopelekea kuhukumiwa kwenda jela miezi 12.
Kijana MOHAMED kabla ya hapo alikuwa akitumikia
kifungo cha miezi tisa (9) jela kwa kosa la kutoroka chini ya ulinzi halali wa
askari wa kituo cha polisi Kipumbwi, kwa kuvunja dirisha la lock up.
No comments