AENDA JELA KWA KUMUIBIA MKE WAKE WILAYANI PANGANI
Mahakama ya mwanzo mwera imetoa hukumu kwa kijana
LUKAS ATHUMAN (29) kwenda jela miezi mitano (5) kwa kukutwa na hatia ya kuvunja
na kuiba godoro moja na mashuka mawili, mali ya mke wake Bi Amina Abdallah.
Hati ya mashtaka inaeleza kuwa kijana Lukas mnamo tarehe 30/6/2016 kijiji cha Kasanga wilayani
Pangani, alitenda kosa la kwanza ambalo ni kuvunja nyumba kwa nia ya kuiba, na
kosa la pili kuiba godoro moja la futi tano kwa sita pamoja na mashuka mawili
mali zenye thamani ya shilingi laki moja na elfu ishirini.
Inadaiwa kuwa kijan Lukas alivizia mke wake huyo
alipokuwa amekwenda katika mizunguko yake ya kila siku majira ya saa 5:00 usiku
na kutekeleza tukio hilo.
Tarehe 21/7/2016 mahakama ya mwanzo Mwera chini ya
Hakimu ANTONY HAMZA ilimuhukumu kijana Lukas kutumikia kifungo cha nje miezi
mitano ambapo alitakiwa kufanya usafi wa maeneo ya zahanati na mahakama.
No comments