WANAFUNZI WA SEKONDARI YA BUSHIRI WILAYANI PANGANI WAFANYA ZIARA PANGANI FM
Wanafunzi wa shule ya sekondari
ya Bushiri iliyopo wilayani Pangani mkoani Tanga wamefanya ziara ya kutembelea kituo
cha redio cha Pangani Fm kwa lengo la kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu tasnia
ya habari.
Wakizungumza kituoni
hapo, mbali na kushukuru uongozi wa Uzikwasa na Pangani Fm kwa maelezo
mazuri ya namna ya upatikanaji wa
habari, wanafunzi hao pia wameeleza
kuwa redio hiyo imekuwa chombo muhimu
kwa wananchi katika kutoa taarifa zinazoendelea
ndani na nje ya wilaya.
Kwa upande
wake mratibu wa
vipindi kutoka Pangani
Fm Bi MARIAMU ALY mbali na
wakuwashukuru wanafunzi hao
kwa ziara ya
kutembelea kituo hicho , lakini pia amewataka kusoma
kwa bidii ili kufikia malengo yao
ya baadae.
Wanafunzi hao
waliambatana na mwalimu wao Twalib Mhando ambaye ni mlezi wa klabu ya Fema
pamoja na mwalimu Richard Mtani ambaye anafundisha wa somo la Kiingereza.
No comments