MBUNGE WA PANGANI JUMAA AWESSO ATEULIWA KUWA NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI

Mbunge wa jimbo la Pangani Mheshimiwa Jumaa Hamidu Awesso ameteuliwa kuwa naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri lililotangaza leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Awesso anakuwa Mbunge wa kwanza kuwa Naibu Waziri kutokea jimbo la Pangani tangu kipindi cha demokrasia ya vyama vingi kuanza nchini Tanzania.

Sambaba na hilo pia Rais Magufuli amemteua Mheshimia George Haruna Mkuchika kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora, ambaye kabla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Mawaziri hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9, 2017, Ikulu jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.