UONGOZI WA KATA YA KIMANG'A WILAYANI PANGANI KUFANYA KIKAO NA WAGANGA WA JADI
Uongozi wa kata ya Kimang’a wilaya ya Pangani kesho unatarajiwa
kufanya kikao na waganga wa jadi ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu
taaluma zao pamoja na kuwatambua kisheria.
Akizungumza na Pangani Mm Afisa mtendaji wa kata
hiyo Bwana Salimu Ugendo Athumani, amesema kuwa wameamua kuitisha kikao na
waganga hao ili kuwaelimisha juu ya sheria na utaratibu zinazowahusu katika
kazi zao.
Katika hatua nyingine Bwana Ugendo amesema, endapo
watawaelimisha na kuwasijili waganga hao, itasaidia kuzingatia uhalali wa njia
na kazi zinazofanywa na kwa kila mgang.
No comments