MHESHIMIWA MAPEPO AAHIDI KUSOMESHA WANAFUNZI WATAKAOFANYA VIZURI KIDATO CHA NNE KATA YA UBANGAA



Diwani wa kata ya ubangaa wilayani Pangani Mheshimiwa  Said Ally Seifu maarufu kama MAPEPO ametoa ahadi ya kuwasomesha wanafunzi wa shule ya secondari ya KILIMANGWIDO watakaofaulu katika mitihani ya kidato cha nne inayotarajiwa kuanza hivi karibuni. 

Mheshimiwa Said Ally Seifu ametoa ahadi hiyo mbele ya wananchi na wanafunzi hao katika mahalafi ya kidato cha nne katika shule hiyo, ambapo alihudhuria kama mgeni rasmi.

Mbali na ahadi hiyo Mhehsimiwa  Said Ally Seifu amesema kuwa, Pangani imepata bahati kwa mbunge wa jimbo hilo Mheshimiwa JUMAA HAMIDU AWESO kuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, hivyo itakuwa rahisi kutatua changamoto ya maji katika maeneo yao.

Ahadi hiyo iliyotolewa na Mheshimiwa  Said Ally Seifu ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Pangani, huenda ikawa chachu kwa wanafunzi hao kufanya vizuri na kuleta hamasa kwa wanafunzi wengine.

No comments

Powered by Blogger.