TIMU YA KIMANG'A YAIBUKA MABINGWA MICHUANO YA AWESSO CUP
Hatimae mashindano ya mpira wa miguu kwa kata
mbalimbali wilayani Pangani ambayo yalikuwa yanadhainiwa na Mheshimiwa JUMAA
HAMIDU AWESO Mbunge wa jimbo la PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
yalimalizika wiki hii katika kata ya BOZA.
Katika mchezo wa fainali ambao ulizikutanisha ya
timu za KIMANG’A na timu ya MNYONGENI, ambapo pamoja na mchezo kuwa mgumu na
kuvutia, lakini mpaka dakika tisini timu ya MNYONGENI ililala kwa bao 5-0.
Awali taarifa zilieleza kwamba Mheshimiwa Jumaa
Hamidu Aweso alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mpambano huo, isipokuwa
kutokana na kuwa na majukumu mapya ya uongozi wake wa nafasi ya Naibu Waziri, alishindwa
kuwasili na hivyo kuwakilishwa na katibu wake Bwana Salimu Bahorera.
Kwa niaba ya Mheshimiwa Awesso, Bwana Bahorera alzungumza
machache tu baada ya kumalizika kwa mpoamabano huo ambapo alisema, ”Kwanza
niwapongeze timu zote mlioshiriki mashindano haya tangu mwanzo hadi leo na
tumefikia tamati, niwaombe tuendelee hivi hivi kwani mchezo ulikuwa wa amani na
utulivu wa hali ya juu pamoja na kwamba timu moja imepoteza kwa goli nyingi
hata namna ambavyo walikuwa wancheza, hakukuwa na ishara yoyote ya uvunjifu wa
amani wala lawama kutoka upande wowote, niseme pia mheshimiwa Mbunge
anawasalimia sana na anasema mkiandaa sherehe za ubingwa basi mumtaarifu
aangalie na ratiba basi ikiwezekana ajumuike nanyi, michezooo oyeeeee”
Kwa upande mwingine msimamizi wa mashindano hayo
Bwana Kayanda Ibrahim amesema ‘’Mashindano haya yanatarajiwa kuendelea tena
kati ya kata za Mwera, Mbulizaga, Mkalamo na hii ni kuelekea katika mashindano
ambayo yatakuja Kujumuisha wilaya nzima kwa kila kata kutoa timu moja ‘’
Katika mashindano hayo ya BOZA ambayo ni mshindi wa
kwanza ilipata Ng’ombe na ziada ya mchele kilo 50 kwa ajili ya sherehe za
ubingwa na mshindi wa pili alipata jezi seti moja moja.
No comments