'SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI' WATOTO WA KIKE WILAYANI PANGANI WATOA NENO!
Wananchi wilayani Pangani wameungana na mikoa
mingine kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani ambapo mambo mbali mbali
yamejadiliwa katika majukwaa ya uwezeshaji watoto hao ikiwemo suala la
kuwapatia muamko wa kielimu.
Wakizungumza na Pangani Fm baadhi ya watoto wa kike
waishio wilayani humo wamesema kuwa, wao kama watoto wa kike wanapaswa kupatiwa
haki zao za msingi ikiwemo elimu, kulindwa na kupatiwa malezi bora yatakayo
wawezesha kutimiza ndoto zao.
Aidha watoto hao pia wamewataka wazazi na walezi
kuweka uwiano sawa katika majukumu kati ya mtoto wa kike na mtoto wa kiume ili
wapate muda wa kujisomea huku wakiwaasa vijana wanaojiingiza kwenye mahusiano
na wanafunzi wa kike waache kwani wanashindwa kutimiza ndoto zao.
Siku ya mtoto wa kike duniani huadhimishwa kila
mwaka ifikapo tarehe 11/10 ambapo kwa
mwaka huu wa 2017 kauli mbiu ya siku hiyo inasema kuwa ‘’KUTOKOMEZA MIMBA ZA
UTOTONI KUELEKEA TANZANIA YA VIWANDA’’
No comments