NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI JUMAA AWESSO AANZA RASMI ZIARA YA KIKAZI MKOANI SHINYANGA

Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la PANGANI Mheshimiwa JUMAA HAMIDU AWESO leo anaanza rasmi ziara ya kikazi mkoani SHINYANGA kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya kimaendeleo maeneo ya MEATU pamoja na MASWA mkoani humo.

Akizungumza na Pangani Fm Radio kwa njia ya simu kutokea Dar es salaam, Naibu Waziri huyo amesema kuwa baada ya ziara hiyo atarudi wilayani PANGANI kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa jimbo lake huku akiomba ushirikiano kwa kipindi chote atakachokuwepo.

Mheshimiwa AWESO amesema kuwa ujio wake utaambatana na timu yake ya wizara ya maji ili kuja kupanga mikakati ya pamoja katika kutatua changamoto ya maji hususani kwa maeneo ambayo yana shida kubwa ya huduma hiyo.

No comments

Powered by Blogger.