BODA BODA PANGANI WALALAMIKIA ABIRIA WAO KUKATAA KUVAA HELMET
Kutokana na kuwekwa utaratibu wa kila Boda Boda kuwa
na kofia ngumu mbili, baadhi ya
waendesha vyombo hivyo wilayani Pangani wameiomba serikali kupitia jeshi la
polisi pamoja na kitengo cha Afya kutoa elimu kwa abiria juu ya umuhimu na
jinsi ya kutumia kofia hizo bila kupata
madhara.
Wakizungumza na Pangani Fm Baadhi ya waendesha Boda
Boda wa mjini Pangani wamesema tangu kuwekwa utaratibu huo asilimia kubwa ya
waendesha Boda Boda wameitikia wito huo wa kuwa na kofia mbila lakini changamoto
wanayoipata ni baadhi ya abiria kukataa kuvaa kofia hiyo wakihofia usalama wa
afya zao.
Aidha waendesha Boda Boda hao wameliomba jeshi la
polisi kukaa na kujadili kwa kina kuhusu matumizi ya kofi mbili kutokana na
changamoto wanazokutana nazo.
Utaratibu wa kila Boda Boda kuwa na kofia ngumu
mbili lilitolewa miezi miwili iliyopita
na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakati akiongea na madareva wa Boda Boda
mkoani Shinyanga ambao walipatiwa
mafunzo ya usalama barabarani mkoani humo ambapo amewataka polisi
kuwakamata madereva hao endapo hawatatii agizo hilo.
No comments