KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KIJIJI MSARAZA YAELEZA MAFANIKIO YAKE BAADA YA KUTEMBELEWA NA UZIKWASA
Kamati ya Kudhibiti Ukimwi ya kijiji cha Msaraza imefanikisha
malengo yake ya kimaendaleo iliyojiwekea ikiwemo kuchangia kambi ya shule pamoja
kuwasaidia makundi maalum ikiwemo watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kuanzia
mwezi Januari hadi mwezi Oktobamwaka 2017.
Wakizungumza na Pangani Fm kamati hiyo imesema kuwa
kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu, moja ya malengo yao makubwa ni
kuhakikisha wanachangia ukuwaji wa elimu unaoenda sambamba na kukuza kiwango
cha ufaulu katika kijiji cha msaraza, ambapo katika kulifanikisha hilo walichangia
kiasi cha shilingi 75,000 taslimu, Mchele Kilo 15, pamoja na magunia sita ya Mahindi
kwa ajili ya kambi ya masomo ya darasa la saba katika shule msingi Bushiri.
Licha ya kiwango hiko cha fedha pia kamati hiyo imejenga
chumba cha darasa la awali katika shule ya msingi Bushiri wakishirikiana na
jamii ya kijiji cha Msaraza.
Kamati hiyo pia imefanikiwa kuwarudisha wanafunzi
watoro sugu shuleni kwa kufanikisha hilo waliunda kamati uliyokuwa na jukumu la
kuwarudisha wanafunzi watoro shule,hadi mwezi October kamati hiyo imefanikiwa
kuwarudisha shule wanafunzi nane kati ya kumi waliokuwa hawahudhurii masomo.
Katika kumuwezesha mwanamke katika uwongozi,wajumbe
wa kamati hiyo wanasema wameweza kuihamasisha jamii kumuona mwanamke kama mtu
imara anayeweza kuiongoza jamii, moja ya matunda ya elimu hiyo ni mwenyekiti wa
kitongoji wa Saanini Bi Amina Nassory, ambaye kwa upande wake amesema jamii
imekuwa ikimpa ushirikiano hata kwenye ngazi ya familia na pia amekuwa akipata
uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa.
Hayo yamejiri katika ufuatiliaji wa mafunzo ya
uongozi wa mguso waliyopewa na shirika lisilo la kiserikali la Uzikwasa kwa
ajili ya kujua mikakati yao ya mwaka mzima, na pia ni kwa kiasi gani wameweza
kuitekeleza mara baada ya mafunzo hayo.
No comments