KIJANA MMOJA AENDA JELA WILAYANI PANGANI KWA KOSA KUMTISHIA MAISHA BOSI WAKE
Mahakama ya mwanzo PANGANI mjini imemuhukumu kijana
EDWARD SHIRIMA mwenye umri wa miaka 33 kwenda jela miezi kumi na tatu au kulipa
faini ya shilingi laki tatu kwa kosa la kutishia kwa maneno.
Hati ya mashtaka iliyowasilishwa na polisi
mahakamani hapo inaeleza kuwa, tarehe 26/8/2017 majira ya saa 7:00 mchana huko
kijiji cha KIGURUSIMBA kijana EDWARD ambaye ni dereva wa tinga alimtishia kwa
maneno bosi wake bwana STEVEN STANSLAUS.
Maelezo ya mahakama yanaeleza kuwa kijana huyo alimwambia bosi wake huyo kuwa anaijua njia
anayopita na watu wake atahakikisha atawaua na baada ya hapo alimwacha bosi
wake akiishi kwa mashaka.
Kulingana na kosa hilo hakimu MGANGA MAGESA ametoa
hukumu kwa kijana huyo kwenda jela miezi 18 au alipe faini ya shilingi laki
tatu kutokana na kijana huyo kukosa pesa ya kulipa faini, na kwa sasa yupo jela
kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi kumi na nane.
No comments