KAMATI ZA VMAC WILAYANI PANGANI ZATAKIWA KUKAMILISHA MIPANGO KAZI YAO
Kamati za kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC Wilayani
Pangani ambazo bado hazijakamilisha utekekezaji wa mipango kazi yao, zimetakiwa
kuutumia muda uliosalia kukamilisha kabla ya kuingia kwenye kilele cha Shindano
la kutafuta kamati bora kwa mwaka 2017.
Akizungumza na Pangani fm Muwezeshaji kutoka shirika
la Uzikwasa Bi Salvata Kalanga, amesema zoezi la ufuatiliaji na tathmini
linalofanywa na shirika la uzikwasa, limetoa taswira ya namna kamati hizo
zinavyotekeleza mipango kazi yao, huku akizitaka kamati ambazo bado
hazijakamisha utekelezaji wake kutokana na vikwazo mbalimbali kutokata tamaa,
na badala yake kutafuta njia mbadala ya kutatua vikwazo hivyo.
Pia Bi Salvata amesema moja ya changamoto iliyoibuliwa
na wajumbe wa kamati hizo ni kusimamishwa kwa watendaji wa vijiji, ambapo
amewataka wajumbe kuacha kulaumu, badala yake kupata funzo jipya kwa lengo la
kuisimamia kamati ipasavyo ili kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.
Katika hatua nyingine kamati ya Kudhibiti Ukimwi Jinsia
nna Uongozi ya kijiji cha Masaika, imesema imefanikiwa kudhibiti tatizo la
mimba Mashuleni, kwa kudhibiti watoto kuingia katika mabanda ya video.
No comments