"HALMASHAURI YA PANGANI IMEJIPANGA KWA ZOEZI LA USAILI"- BI MWANAIDI RAMADHANI NONDO
Afisa Utumishi Wilayani Pangani Bi Mwanaidi
Ramadhani Nondo amesema kuwa Halmashauri hiyo imejipanga vyema kwa ajili ya
usaili wa nafasi za Watendaji wa vijiji pamoja na Makatibu Muhtasi
utakaofanyika siku ya Jumamosi ya terehe 14 hadi 15 mwezi huu wa kumi.
Akizungumza na Pangani Fm mapema leo, Bi Mwanaidi
amesema kuwa wanatengemea kupata maombi mengi kutoka kwa wananchi wenye vigezo kutokana
na matangazo mengi ambayo yamesambaza maeneo mbali mbali.
“Ni matumaini yetu watakuja watu wengi, kwa kuwa pia
tumeweka matangazo kwenye tovuti yetu ya Halmashauri, mbao za matangazo pamoja
na kata zote za wilaya” alisema Bi Mwanaidi.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa, kwa upade wa
mwenyekiti wa bodi ya ajira wameshapeleka mapendekezo kwenye kamati ya fedha na
kwa sasa wanasubiri baraza la Madiwani kupitisha huku akiwataka wananchi
kutarajia usaili wa haki.
No comments