VMAC KIJIJI CHA MIVUMONI YAENDELEA KUTEKELEZA MIPANGO YAKE YA KIMAENDELEO
Kamati ya Kudhibiti Ukimwi ya kijiji cha Mivumoni imetekeleza
baadhi ya malengo yake ya Kimaendeleo iliojiwekea kuanzia mwezi Januari mpaka
Oktoba, ikiwemo kuchangia ujenzi wa majengo ya shule pamoja na kuzisogeza
karibu huduma muhimu za kibinadamu ikiwemo maji kijijini hapo.
Wakizungumza na wawakilishi kutokea shirika la UZIKWASA,
wanakamati hao wamesema kuwa katika kipindi chote cha mwaka 2017 kuanzia mwezi
Januari hadi mwezi Oktoba, wameweza kushirikiana na serikali kujenga vyoo vya
shule, pamoja na kutengeneza matofari kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya shule
kwa madhumuni ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa amani.
Wajumbe hao pia waliweza kuchangia Mchele Kilo 28
kwa ajili ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba wakati wakifanya mtihani wao
wa mwisho.
Licha ya hayo, Kamati hiyo kwa kushirikiana na
Uwongozi wa shule ya msingi Mivumoni wamewarudisha shule wanafunzi wawili ambao
waliokuwa wanasoma darasa la pili wa jinsia ya kike ambao hapo awali walikuwa
ni watoro na hadi hivi sasa wanaendelea na masomo shuleni hapo.
No comments