MWANAMKE AKUTWA AMENYONGWA KIJIJI CHA MWERA WILAYANI PANGANI



Mwili wa mkazi wa kitongoji cha Mabatini kijiji cha Mwera wilayani Pangani aliyefahamika kwa jina la Kibibi Mohammed umekutwa umenyongwa kwa kutumia mtandio huku baadhi ya sehemu zake za mwili zikiwa zimekatwa.

Akithibitisha kutoka kwa tukio hilo Kaimu Mkuu wa jeshi la polisi wilayani ASP MAYASA OMARY amesema kuwa, mnamo tarehe 20/10/2017 majira ya saa kumi jioni, walipata taarifa kwa njia ya simu ya mkonini kutokea kijiji cha Mwere kuhusu tukio hilo.


“Taarifa ni kuwa katika kitongoji cha Mabatini kata cha Mwera, kulionekana mwili wa marehemu Kibibi Mohammed Ibrahim mwenye umri wa miaka 16 kabila la Mzigua, ukiwa umenyongwa kwa kutumia mtandio huku masikio yake yote mawili yakiwa yamekatwa” alisema ASP Mayasa.

ASP Mayasa ameongeza kwa kusema kuwa, mbali na viungo hivyo kukatwa pia nywele za marehemu zilikutwa zimenyolewa, huku mwili wake ukikutwa kichakani, takribani mita 25 kutoka nyumba aliyokuwa anaishi na mume wake.

Mpaka sasa jeshi la polisi wilayani Pangani linamshikilia mume wa marehemu kwa ajili ya uchungizi zaidi.

No comments

Powered by Blogger.