JESHI LA POLISI (W) PANGANI LATHIBITISHA KUPATIKANA KWA MAITI NYENGINE YA WAVUVI WALIOZAMA BAHARINI
Siku moja baada ya
jeshi la polisi wilayani Pangani kutangaza kupotea kwa watu wanne kwenye bahari
hindi baada ya Boti ya uvuvi iliyokuwa na jumla ya watu 17 kuzama, ambapo
kwenye taarifa ya awali ilieleza kuwa mtu mmoja alifariki, 12 kuokolewa, leo
tena mtu mwengine amepatikana amefariki dunia ikiwa ni miongoni mwa wale wanne.
Kijana aliyepatikana
ametambulika kwa jina la MOHAMED YUSUPH anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 29, ambapo
mwili wake umepatikana ukiwa unaelea juu
ya maji katika maeneo ya Kokoni nje kidogo ya mji wa Pangani.
Akithibitisha
kupatikana kwa mwili huo Kaimu Kamanda wa Polisi ambae ni mkuu wa kituo cha Polisi
wilayani Pangani ASP MAYASA OMARY, amesema kuwa kutokana na tukio la Boti
kuzama hapo jana mapema leo hii
wamefanikiwa kupata mwili mmoja ambao unakamilisha idadi ya watu wawili
waliofariki dunia ambapo mpaka sasa watu
watatu bado hawajapatikana.
“Mwili umehifadhiwa
katika hospitali ya wilaya hapa Pangani kwa ajili ya kuwasubiri ndugu wa
marehemu, waje na kufanya taratibu za mazishi.” Alisema Mayasa
Kwa upande wake Mganga
Mfawidhi wa hospital ya wilaya ya Pangani KOMBO MUHINA, mbali na kukiri kupokea
majeruhi 12 hapo jana, lakini pia leo amekiri kupokea mwili wa kijana Mohammed
Yusufu ili kusubiri ndugu zake.
Hadi
sasa inaelezwa kuwa watu watatu hawajapatikana mara
baada ya chombo walichokuwa wakikitumia katika shughuli za uvuvi kupata dhoruba
katika mkondo wa bahari ya hindi wilayani Pangani hapo jana.
No comments