WAKUU WA IDARA WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUWEKA NGUVU KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO YA HALMASHAURI HIYO
Wakuu wa idara na wataalamu mbali mbali katika
halmshauri ya wilaya ya pangani wametakiwa kuweka nguvu ya kutosha katika ukusanyaji wa
mapato na usimamizi wa miradi ya maendeleo ili kuiweka salama halmashauri hiyo.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani
mapema leo mkuu wa wialaya ya Pangani bi zainab abdallah issa amesema
halmshauri imejaa ukiritimba katika ukusanyaji wa mapato hali ambayo inaatarisha
wilaya kufutwa kutokana na kudorora katika usimamizi wa miradi ya kimaendeleo kunakopelekea
wilaya kukosa mapato ya kutosha.
‘’Tulitazame hili eneo as a seriase ajenda, itafikia
mahala serikali itasema tuifunge hii halmashauri imeshindwa kufikia malengo na
kusababisha wataalamu kufa kifo cha mende, sasa ifike mahala kilammoja aguswe
katika ukusanyaji kodi’’amesema bi zainabu.
Aidha bi zainabu ametaka kikao hicho
kilichowakutanisha wakuu wa idara, mkurugenzi wa halmshauri hiyo, madiwani na
wadau mbali mbali wa kimaendeleo kutoka ndani na nje ya wilaya, kitumike katika
kutafakari na kutoa muelekeo wa namna gani ukusanyaji wa mapato utapanda kuliko
ilivyosasa.
‘’ kama halmashauri inafikia mahala badala ya
kupanda inashuka ni lazima tujitathimini, kwani halmashauri hii haina vyanzo
vya mapato jamani? Mpaka tunabeba madeni mengi? Nawaachia home work na
kukubaliana mikakati ya ukusanyaji wa mapato'' amesema bi zainabu
Wakati huo huo mkuu wa wilaya huyo ameonekana
kukerwa na swala la usimamizi wa miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa katika
halmashauri hiyo ambapo fedha za miradi wilayani humo hutumika kinyume na
utaratibu.
Bi ZAINABU amezungumzia swala la ujenzi wa ukingo wa
mto pangani unaogharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 2.4 na upandaji wa
mikoko unaogharimu milioni 45, ambapo fedha zilizoelekezwa katika upandaji wa
mikoko imedaiwa kutumika kinyume na taratibu, hali iliyoibua sinto fahamu ya
vipi zilivyotumika na nani aliyeidhinisha matumizi hayo.
‘’mradi hule wa ujenzi wa ukuta upo katika hatua hizi
mbili, hatua ya kwanza ujenzi wa ukuta wenyewe na mradi wa pili ni upandaji wa
mikoko, tulipewa maelekezo na wizara tupande miti ya mikoko isiyopungua elfu 21
lakini kwenye mchakato ikagundulika kuwa kikao hiki cha baraza kiliidhinisha
zile pesa zitumike katika shughuli nyingine’’amesema bi zainabu
Mnamo October 12 mwaka huu 2017 waziri wa nchi ofisi
ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa muheshimiwa SULEIMANI JAFFO
alizitaka halmashauri zilizokopa kwa ajili ya shughuli za mbali mbali za
kimaendeleo kutoka kwenye bodi ya mikopo ya serikali za mitaa kuhakikisha
wanarejesha fedha hizo kabla ya disemba 2017 huku akizitaja halmshauri 9 sugu
katika deni hilo ikiwemo halmashauri ya wilaya ya pangani.
No comments