BOTI YA UVUVI YAZAMA NA KUUA MTU MMOJA WILAYANI PANGANI HUKU WENGINE WANNE HAWAJULIKANI WALIPO
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne hawajulikana
walipo mara baada ya chombo walichokuwa wakikitumia katika shughuli za uvuvi
kupata dhuruba katika mkondo wa bahari ya hindi wilayani Pangani.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo afisa mpelelezi
kutokea wilayani Pangani ASP Matiku amemtaja aliefariki dunia kuwa ni Jumanne Abdallah
mwenye umri wa miaka 18.
“Aliyefariki ni mkazi wa Shakani huko Zanzibar,
lakini pia mpaka sasa watu waliookolewa ni 12 ambao wamethibitishwa, nah ii imetokana
na dhoruba kubwa ya mawimbi baada ya bahari kuchafuka, matokeo yake chombo chao
kikapigwa wimbi na kuzama” alisema Matiku.
Matiku ameongeza kwa kusema kuwa, amezungumza pia na
mmiliki wa chombo hicho Bwana Mohammed Mzee, na kulieleza jeshi la polisi kuwa
jumla ya watu waliokuwepo ndani ya chombo hizho ni 17.
No comments