"WANANCHI WA PANGANI WANAPASWA KUTUNZA UOTO WA ASILI"- DAUDI MLAHAGWA
Wananchi wilayani Pangani wametakiwa kutunza uoto wa
asili katika fukwe za bahari ili kupunguza kasi ya kusogea kwa bahari ambayo
inatokana na kuliwa kwa ufukwe huo.
Agizo hilo limetolewa na Afisa Mazingira Wilaya ya
Pangani Bwana Daudi Mlahagwa ambapo mbali na hilo lakini pia amesisitiza kuwa
wananchi wanapaswa kuuheshimu uoto huo ikiwemo Milakasa ili kuzuia bahari isiendelee
kumeza ardhi kwa kuwa hali ilivyo sasa
inatishia kutoweka kwa mjini wa Pangani kutokana na kusogea kwa bahari hiyo.
Katika hatua nyingine Bwana Mlahagwa amesema kuwa
kutokana na kasi hiyo ya bahari kusogesa karibu na mji wa Pangani jitihada
walizozifanya ni kuendelea kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira na rasilimali
za bahari pamoja na kuwaalika viongozi
wakubwa wa serikali akiwemo Mheshimiwa Januari Mamkamba ambaye Mazingira na
Muungano ili kusaidia ujenzi wa ukuta katika ufukwe huo.
Kasi ya kuliwa kwa fukwe za bahari imekuwa
ikiongezeka siku hadi siku na kuzua hofu ya kuzama kwa mji wa Pangani, lakini
tayari serikali imeonyesha nia ya kudhibiti hali hiyo.
No comments