MKUTANO WA KIJIJI PANGANI MASHARIKI WAAHIRISHWA BAADA YA KUTOFIKIA MAKUBALIANO
Suala la ugawaji wa maeneo katika eneo la Gombero
katika kijiji cha Pangani Mashariki limeendelea kuchukua sura mpya kila kukicha
baada ya mkutano wa kijiji uliofanyika jana kuahirishwa baada ya kutofikia
makubaliano.
Katika mkutano huo uliofanyika katika eneo la Funguni
mjini Pangani hoja kubwa ilikuwa ni juu ya mamlaka ya utoaji wa viwanja katika
eneo la Gombero, huku baadhi ya wanachi wakitoa maoni yao juu ya suala hilo.
Kwa upande wake Afisa Mipango Miji kutokea
halmashauri ya Pangani alibainisha juu ya umiliki wa eneo hilo la kijiji cha
Pangani Mashariki, hasa katika eneo la Gombero.
“Yale maeneo yote ambayo yametangazwa kama ni ya
upangaji, ikiwemo eneo la Pangani Mashariki, maeneo hayo yanakuwa chini ya
Kamishna, kwa halmashauri Mkurugenzi ndio anakuwa amekasimiwa, kwa hiyo masuala
ya mipango miji yanakuwa yana sheria zake, ndio maana katika suala hili sheria
inayotumika ni ile sheria namba 4 ya mwaka 1999 na sheria namba 8 ya mwaka 2007
ya mipango miji” Alisema.
Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Bwana Sabas Damian Chambasi ulioanza majira
ya saa nane mchana na kulimalizika majira ya saa kumi na mbili jioni lakini panoja na yote hayo bado hakuna
maazimio yoyote ambayo yalifikiwa na hivyo kuahirishwa mpaka hapo utahapokuja
tajwa tena.
Hii ni baada ya wanachi kutoridhika na ugawaji wa
viwanja ambapo wamesema wanahitaji jukumu hilo libakie ndani ya kijiji cha
Pangani Mashariki.
No comments