AMBONI PLANTATION WILAYANI PANGANI YASAIDIA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SHULE YA MSINGI KIPUMBWI WILAYANI HUMO.
Pichi hii sio halisi ya jengo
Uongozi wa shule ya msingi kipumbwi wilayani Pangani
imeshukuru uongozi wa kampuni ya AMBONI PLANTATION wilayani humo kwa kujitolea
kukarabati madarasa matatu shuleni hapo.
Akitoa shukrani hizo alipotembelewa na kituo cha
pangani fm radio shuleni hapo Mwalimu Damian Machila ambaye ni mkuu wa shule
hiyo mbali na kutoa shukrani zake pia amesema madarasa hayo yatasaidia sana
kwani hapo awali walikuwa na madarasa matano tu hali inayosababisha watoto
kukaa wengi darasa moja.
‘’Kwa
kweli tunayo furaha kubwa kwa kupata uyu mfadhili wa kutukarabatia majengo haya
matatu yaliyokuwa mabovu sana hasa kwenye paa na sakafu, ukitazama idadi kubwa
ya watoto tulio nao, tuna watoto zaidi ya 195, kwa shule ya msingi na idadi ya
154 kwa shule ya cheke chea. Namshukuru sana meneja wa amboni plantation kwa
moyo aliouonyesha kwani ameyakarabati kwa kiwango cha hali ya juu sana’’
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo
bwana SAMWEL DENIS ametoa shukrani na kueleza jinsi madarasa hayo
yalivyokarabatiwa kwa kwa viwango na usalama wa wanafunzi wawapo darasani.
Katika hatua nyingine bwana SAMWELI amesema licha ya
ukarabati huo, bado kuna uhitaji wa ukarabati wa nyumba ya walimu na vyoo vya
wanafunzi hivyo ameomba wadau wa elimu na wawekezaji kusaidia shule hiyo.
‘’Bado
tunaangaika kutafuta wafadhili wengine kama tanapa, wawekezaji wa minara ya
simu, tunaomba wafadhili wajitokeze ili kutusaidia ukarabati wa nyumba za
walimu na vyoo.amesema denis’’
Shule ya msingi Kipumbwi ni moja ya shule
inayokabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo madarasa, vyoo, nyumba za
walimu na upungufu wa walimu ambao hadi sasa bado haijafikia hata asilimia 50
ya hitaji la walimu shuleni hapo.
No comments