MHESHIMIWA AWESSO ATOA POLE KIFO CHA DIWANI MAJIRA



Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni mbunge wa jimbo la pangani muheshimiwa jumaa hamidu aweso atoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na watu waliofanya kazi kwa karibu na Marehemu Saidi Mohammedi Majira aliyekuwa Diwani wa Kata ya Madanga katika Wilaya ya Pangani.

Akizungumza na kituo hiki Muheshimiwa Aweso akiwa safarini Songea, amesema kuwa taarifa za kifo cha Ndugu Majira zimeleta mshtuko katika nyoyo za walio wengi kutokana na namna alivyokuwa akishirikiana na watu katika kufanikisha mambo mbali mbali.

Aidha Muheshimiwa Jumaa Aweso amesema "kuondoka kwa Majira ni pengo kwa Halmashauri, hivyo nawaomba wananchi wa kata ya Madanga kuwa na subra na kuendeleza mshikamano katika kipindi hiki cha majonzi.
Pia ningeomba wananchi kujitokeza kwa wingi hapo kesho katika kijiji cha Ushongo kumsindikiza Ndugu yetu Saidi Mohammedi Majira."amesema
mbunge wa jimbo la pangani Jumaa Hamidu Aweso

No comments

Powered by Blogger.