WALIMU SHULE YA MSINGI MIKINGUNI WILAYANI PANGANI WAASWA KUFANYA KAZI KWA BIDII
Wito umetolewa kwa walimu wa shule ya msingi
MIKINGUNI wilayani pangani kufanyakazi kwa bidii na kujitolea kwa moyo wa
kuwafundisha wanafunzi ili waweze kuwa chachu ya mafanikio katika kijiji cha
MIKINGUNI wilayani humo.
Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti wa kamati ya shule
hiyo bwana WAZIRI MBEZI na kuongeza kuwa wazazi wasiwaozeshe watoto wakiwa na
umri mdogo wawaache wasome kwanza hayo mambo mengine yatafuata baadae.
‘’wazazi wamekuwa
na tabia ya kuwalimbikia watoto wa kike kazi za nyumbani hii haisaidii
kunyanyua motto huyu kielimu, hapo hapo atakapo fanya vibaya ndo mzazi unakuwa
kipaimbele kumuozesha, tunatakiwa kubadilika wanamikinguni’’ amesema mbezi.
Bwana WAZIRI amesema kuwa mkwamo uliopo ni utoro kwa
wanafunzi jambo linaloitaji ushirikiano kati ya walimu na wazazi ili kuuondoa.
‘’Kwa mwaka
huu wa 2017 matokeo angalau yametoka mazuri, lakini mkwamo uliokuwepo ni swala
la utaro wa reja reja kwa wanafunzi, naamini tukishirikiana kati ya walimu na
wazazi ili swala litaondoka’amesema bwana waziri
No comments