USHIRIKIANO CHACHU YA MAENDELEO VMAC KIJIJI CHA MSARAZA
Ushirikiano na Umoja ni miongoni mwa sababu
zinazotajwa kuongeza ari ya Uwajibikaji kwa viongozi katika kijiji cha MSARAZA,
hasa kwenye nyanja za kimaendeleo na ukatili wa kijinsia.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wajumbe wa
kamati ya Kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC ya kijiji cha MSARAZA kata ya
BUSHIRI Wilayani PANGANI, wamesema kuwa hatua kubwa ya maendeleo waliyopiga
hadi sasa ni kutokana na ushirikiano waliojidhatiti ili kufikia lengo
walilokusudia.
‘’Kikubwa
ninachojivunia ni mshikamano, umoja wetu na makubaliano na kujitoa kwa hali na
mali jambo linalochochea maendeleo’’ Alisema mwanakamati.
Wajumbe hao wameongeza kuwa mafanikio hayo
yametokana na ushirikiano baina yao jamii na wadau mbalimbali, na kwamba suala
hilo limesaidia kuwa kitu kimoja katika kila shughuli.
‘’tunashirikiana
na jamii mfano vikundi mbali mbali wadau wengine wa kielimu, hatupo vimac peke
ake tunashirikiana na wakina mama, wauguzi wetu kitu ambacho imetuweka pazuri
na jamii inayotuzunguka’’ amesema mwanakamati
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji na Mwenyekiti
wa kamati ya VMAC Msaraza Bwana Hemedi Daudi Kiwonike, amesema kuwa mafanio
yote ni baada ya kupata elimu ya mguso iliyowawezesha kuibua changamoto na
kuweza kuzitatua.
‘’mafunzo ya
uongozi wa mguso yanayotolewa na shirika la uzikwasa yametufanya kila
kinachotokea katika kijiji chetu tunakuwa tunashikamana na tunashirikiana kama
ni tatizo tunaakikisha tunalitatua kwa pamoja’’ Alisema mwenyekiti
Kamati za Kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC za
vijiji Wilayani Pangani, kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiibua na kubuni shughuli
mbalimbali za kimaendeleo, huku zikipiga hambushi katika masuala ya jinsia na
uongozi.
No comments