MAMIA WAJITOKEZA MAZISHI YA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA MADANGA SAIDI MAJIRA



Baadhi ya wakazi wa wilayani pangani wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Madanga wilayani Pangani  Bwana Saidi Mohammedi Majira.

Akitoa pole kwa wanafamilia na wananchi waliohudhuria katika mazishi hayo Mwenye kiti wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Bwana SEFU ALLY MAPEPO amesema kuwa marehemu ameacha pengo ambalo ni gumu kuzibika kwani walimtegemea sana kwa ushauri kutokana na busara zake.

Aidha kwa  upande wa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo bwana      SABASI DAMIAN CHAMBASI akitoa wasifu wake amesema  marehemu alikua akiitumikia halmashauri ya wilaya Pangani kwa vyoo tofauti tofauti kwa kipindi cha miaka nane kutokana na weledi wake katika kazi, hadi alipofikwa na umauti katika hospitali ya taifa ya muhimbili jijini Dar Es Salaam.

Marehemu saidi mohammedi majira amefariki akiwa na umri wa miaka 65 na kuacha mke mmoja na watoto tisa,na amezikwa  huko katika kijiji cha Ushong mabaoni, wilayani Pangani.

Katika maziko hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikalini,viongozi wa dini na viongozi wa vyama tofauti.

baadhi ya viongozi wakiuaga mwili wa marehemu
Saidi Mohammedi Majira

 Wananchi wakisikiliza wasifu wa marehemu Saidi Mohammedi Majira



No comments

Powered by Blogger.